Saturday, July 11, 2015

Maneno 36 ya Waziri Membe Kuhusu Mtu Aliyekamatwa na Mabilioni ya Wajumbe Dodoma..


Kuna stori zimeenea mitandaoni kwamba kuna mtu ambae amekamatwa na mabilioni ya pesa Dodoma, kingine ni kwamba amekamatwa na simu ikiwa na maelekezo kwamba pesa hizo ni za kuwapatia Wajumbe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ameandika ujumbe @Twitter kukanusha kuhusika na mtu huyo


  • “Kuna taarifa za uongo zinazoenezwa kwamba kuna “Mtu wa Membe” amekamatwa na pesa Dodoma“


Kwenye Tweet nyingine Waziri Membe ameandika hivi

  • ”siasa hizi ni za hovyo kwani hazitajenga Taifa letu. Naomba msihadaike na watu wanaotaka kututia doa baada ya kukosa uchafu dhidi yetu”  @BernardMembe