Saturday, September 8, 2012
UTAFITI WA USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI WA BARABARANI KATIKA TARAFA YA KAMACHUMU
MOJA YA GARI NDOGO HUTUMIKA KATIKA KAMACHUMU
Pikipiki pia zinatumika kama usafiri kamachumu
Wakazi wengi wa mji wa tarafa ya kamachumu ambayo inapatikana katika wilaya ya Muleba kaskazini wanamiliki vyombo vya usafiri kama vile pikipiki,baiskeli na magari ingawa wamiliki ni wachache. Katika suala la kuzingatia sheria za usalama wa barabarani limeenda likizo kwa wengi wa miliki wa vyombo vya usafiri wa barabarani kwa wachache ndio wanazingatia sheria za barabarani. Madereva wa vibasi vidogo vifanyavyo safari ya kutoka kamachumu kwenda mjini Bukoba hawazingati kanuni za usalama barabarani wanaendesha kwa mwendo wa kasi magari yao bila kujali kama wamebeba abiria ndani ya magari wanayoendesha na abiria nao hata wajali usalama wa usafiri wao wenyewe bora wafike. Tukija kwenye masuala ya usalama wa usafiri wa chombo cha baiskeli wakati wa majira usiku ndio shaghalabaghala kabisa,kutokana na baiskeli nyingi hazina taa za kuwaongoza usiku.kibaya zaidi wanapenda kuziendesha wakati wa usiku bila kuogopa usalama wao kama vile kupata ajali za kuwaletea ulemavu wa viungo vya miili yao. Inabidi polisi wa usa usalama barabarani katika tarafa ya kamachumu wachukue hatua za haraka kudhibiti hali ya usalama wa barabarani ili taifa liepuke majanga ya ajali za barabarani. Kinga ni bora kuliko tiba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment