Wednesday, November 14, 2012

Matumizi ya maziwa ya ngamia yaongeza ukuaji wa uchumi katika vijiji vya Kenya

Kila asubuhi, kijiji kidogo sana cha Ukasi katika wilaya ya Tana River ya Kenya kinakuwa katika msisimko wa harakati.
  • Wachungaji wakileta ngamia wao kunywa maji katika wilaya ya Wajir. [Bosire Boniface/Sabahi] Wachungaji wakileta ngamia wao kunywa maji katika wilaya ya Wajir. [Bosire Boniface/Sabahi]
  • Lori lililojazwa makontena yenye maziwa ya ngamia huko Garissa. Kuongezeka kwa matumizi ya maziwa ya ngamia kumeongeza tena hamu ya kumfuga mnyama huyo. [Bosire Boniface/Sabahi] Lori lililojazwa makontena yenye maziwa ya ngamia huko Garissa. Kuongezeka kwa matumizi ya maziwa ya ngamia kumeongeza tena hamu ya kumfuga mnyama huyo. [Bosire Boniface/Sabahi]
Kati ya saa 11 asubuhi hadi saa sita mchana, watu katika kijiji hiki hukutana katika soko lililo katika eneo hilo kujaza makontena ya lita tatu na lita 20 kwa maziwa ya ngamia kwa maandalizi usafiri. Wanaume na wanawake wanakaa na madaftari , kunukuu kwa uangalifu kiasi cha lita, bei na tarakimu nyingine.
Zahara Yussuf Abdi, mwenye umri wa miaka 48, mkaazi wa eneo hilo na mfanyabiashara wa maziwa, alisema kijiji hicho kimejulikana kama kituo cha maziwa ya ngamia.
"Tunanunua maziwa kutoka kwa wafugaji kutoka katika vijiji vya mbali na kusambaza zaidi ya lita 5,000 za maziwa kwenda Nairobi na Garissa kila siku," aliiambia Sabahi. "Ni lazima tutembee kwenda kutafuta magari ya binafsi au yanayohudumia umma kueleka katika miji hiyo kupeleka maziwa ndani ya saa 12 kutoka maziwa yalipokamuliwa."
Mwishoni mwa mwezi, familia nyingi zinapata zaidi ya shilingi 50,000 (dola 585) kutokana na biashara hii, alisema. Kwa viliyokuwa vijiji vilivyokuwa nyuma katika jimbo la Kaskazini Mashariki vimepata nguvu mpya kutokana na mahitaji ambayo hayajawahi kutokea ya maziwa na nyama ya ngamia.
Ofisa wa Uzalishaji wa Mifugo wa Wilaya ya Wajir Omar Bulle alisema matumizi ya maziwa na nyama ya ngamia imekuwa kwa zaidi ya asilimia 10 kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita,ikiwaingizia wafugaji mapato makubwa zaidi.
"Katika baadhi ya miji, maziwa ya ngamia yamechukua nafasi ya maziwa ya ng'ombe," alisema, akiongeza kwamba ongezeko hilo limewezekana kwa sababu mahitaji yameongezeka kupita kwa Wasomali wa Kenya, ambao wamekuwa wateja wa kwanza.
"Mahitaji hayo pia yamechochea hamasa ya wafugaji kuendelea na mifugo, ambayo wakati fulani walionekana kuitelekeza kutokana na upataji mdogo wa faida," Bulle alisema.
Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2008 uliyofanywa na Kituo cha Kutafuta Rasilimali uliyoandaliwa na Shirika la Maendeleo la Netherlands, uzalishaji wa maziwa ya ngamia nchini Kenya mwaka 2007 ulikadiriwa kuzidi takriban lita milioni 340, zilizokuwa na thamani ya shilingi bilioni 8 (dola milioni 94).
Ni asilimia 12 tu ya maziwa, kiasi cha lita milioni 40, kiliuzwa katika soko, utafiti uligundua. Kwa iliyobakia, asilimia 38 ilitumiwa na wafugaji na mengine kupotea.
Hata hivyo, katika miaka miwili iliyopita, serikali ilisema upoteaji umepunguzwa. Waziri wa Maendeleo ya Mikoa Fred Gumo alisema zaidi ya lita milioni 80 za maziwa ya ngamia zinauzwa kwa mwaka. "Sekta inaingiza zaidi ya shilingi bilioni 12 kwa mwaka," aliiambia Sabahi.
Kuleta ongezeko zaidi, serikali iko katika hatua ya kuanzisha mashamba madogo ya ngamia wa maziwa katika mikoa inayofuga ngamia, Gumo alisema. Zaidi ya hilo, serikali na wabia wa maendeleo wanashirikiana kukarabati miundombinu ya soko na kupambana na magonjwa ya mifugo.

Mahitaji yasiyokuwa na mfano ya maziwa ya ngamia

Kampuni ya Vital Camel Milk Limited iliyoko Nayuki, ambayo inadaiwa kuwa mtambo wa kwanza duniani kwa ajili ya kuzalisha maziwa ya ngamia, ilisema mauzo yameongezeka sana kwa miaka mitatu iliyopita.
"Tumeona mauzo yakikua kutoka asilimia 15 hadi 20 mwaka baada ya mwaka tangu tulipoanza mwaka 2005 na tunatarajia kuongezeka kwa kadiri tunavyoendelea kujipanua katika mkoa na watu wamegundua faida ya maziwa ya ngamia," alisema Holger Marbach, mmiliki wa mtambo wa maziwa.
Alisema mahitaji pia yanaongezeka katika nchi nyingine za Afrika Mashariki, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini.
Mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kusimamisha uzalishaji wa maziwa ya ng'ombe au kuua mifugo, ngamia wana uwezo wa kuzalisha maziwa karibu mwaka mzima, alisema Yusuf Abdullahi, mwenyekiti wa tawi la Wajir la Baraza la Masoko ya Mifugo Kenya.
Serikali inaweza baadaye kusaidia uzalishaji kwa kutoa magari ya mizigo yenye mafriji kwa ajili ya kusafirisha maziwa na kuwafundisha wafugaji kutafuta masoko na kuzalisha bidhaa, aliiambia Sabahi.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, maziwa ya ngamia yana ladha ya chumvi kidogo kuliko ya ng'ombe na yana vitamini C mara tatu zaidi. Pia yana vitamini nyingine nyingi zaidi, mafuta kidogo na yana asidi mafuta sikifu ya kutosha.
Elphus Muka, mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa Busia katika Mkoa wa Magharibi, alisema kuna fursa za kuongeza matumizi kote nchini, kwani watu wengi wanaendelea kutoelewa faida za maziwa ya ngamia kwa sababu ya utangazaji mbovu wa masoko.
"Sijawahi kufikiria kwamba maziwa na nyama ya ngamia vinaweza kuliwa hadi niliposoma faida zake za afya na tiba," aliiambia Sabahi. Alisema familia na marafiki zake sasa wamekuwa watumiaji wa kila mara.
Source: http://sabahionline.com/swahili

No comments:

Post a Comment