Tuesday, November 13, 2012

Polisi 40 wauawa na wezi wa mifugo Kenya


 kriban polisi 40 wamethibitishwa kuuawa nchini Kenya katika shambulizi lililofanywa dhidi yao siku ya Jumamosi walipokuwa wanajaribu kuokoa mifugo waliokuwa wameibwa.
Maafisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, kaunti ya Samburu, Kaskazini mwa nchi
Msemaji wa polisi aliambia BBC kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na washambuliji watatu , lakini viongozi wa kijiji wanahofia kuwa huenda maiti zaidi wakapatikana. Hii leo miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya polisi waliouawa kuwa 40.
Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya uhaba wa malisho ya mifugo wao
Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.
Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake.
Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana Jumapili.

Ramani ya Kenya
Inspekta wawili wakuu wa polisi wangali hawajulikani waliko.
Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya polisi waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura tisa wangali wanapokea matibabu hospitalini.
Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo katika wiki mbili zilizopita hadi 43.
Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri inspekta mkuu wa polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu ya mzozo wa mishahara.
Source:BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment