Almasi zenye thamani ya dola bilioni 1.25 zimeibwa nchini
Zimbabwe. Kulingana na shirika la Partnership Africa Canada (PAC)
Shirika hilo linasema kuwa huu ndio wizi wa hali
ya juu wa Almasi kuwahi kufanywa tangu enzi ya Muingereza Cecil Rhodes
aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri wa Almasi.Shirika hilo linadai kuwa wizi huo uliofanywa katika mgodi wa Almasi wa Marange, uliwanufaisha maafisa wa Zimbabwe, wafanyakazi wa kimataifa wa madini na makundi ya wahalifu.
Afisaa mmoja katika sekta ya madini nchini humo, alipuuza madai hayo akasema kuwa ni uongo mtupu.
Ripoti ya shirika hilo ijulikanayo kama, "Reap What You Sow'' ufisadi na uporaji katika mgodi wa Marange, ilitolewa na shirika hilo la nchini Canada, ikinuiwa kwenda sambamba na mkutano wa serikali kuhusu biashara ya Almasi.
Ukiukwaji mkubwa wa sheria.
Rais Robert Mugabe, katika hotuba yake kwa wajumbe alisema kuwa serikali itazingatia sana sheria za kimataifa kuhusu uchimbaji wa Almasi , uhifadhi na uuzaji wake.
Marufuku hiyo iliwekwa mwaka 2009, kufuatia mauaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu katika mgodi wa Almasi wa Marange pamoja na ripoti kuwa maafisa wa kijeshi walikuwa wanajinufaisha na biashara haramu
Shirika la PAC lilisema kuwa ukiukwaji huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kutisha.
''Tunakadiria kuwa almasi za thamani ya dola bilioni mbili ziliibwa tangu mwaka 2008'' shirika hilo liliongeza.
Mwezi Julai waziri wa fedha wa Zimbabwe Tendai Biti alisema kuwa nchi hiyo inatarajiwa kupata dola milioni miasita kama mapato ya kigeni kutokana na mauzo ya Almasi nje ya nchi lakini waliweza kupata tu milioni arobaini na sita.
source:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment