Monday, October 20, 2014

Scandal Miss Tanzania 2014 , she Suck for crowned

Miss Tanzania with First Runner up, Lilian Kamazima and second runner up Jihan.  
Luck was on her side that night, but misfortune soon came knocking with it.
 

 IMG-20141016-WA0008 
Her passport states she was born in 1989. That makes her 25 this year and 26 in 2015 when she will represent the country at the Miss World competitions.
As any other big names invasion of privacy is common. Someone had to prove wrong the Miss Tanzania committee.
First it was her size, most people said she was oversized unfit for the beauty pageant. Then it was her age; she was registered as an 18 old but it has been proved otherwise.

  

Monday, October 13, 2014

MAGADASHI MC MKALI WA MWANZA ATOA WIMBO MPYA MAPITO AMSHIRIKISHA INO BIZLE

 
 Anajulikana kama Joas Julius Magadula, kwa jina la kisanii anaitwa MAGADASHI MC, mkali kutoka jiji la mwanza ambaye aliibuka kama mshindi wa free style competition mwaka jana na kujinyakulia zawadi ya kurekodi nyimbo tatu na promo ya miezi sita, Madashi ameachia pini lake jipya akimshirikisha INO BIZLE

Tuesday, July 23, 2013

ONLY IN TANZANIA: Tsvangirai aandamwa na kashfa huku uchaguzi ukikar...

ONLY IN TANZANIA: Tsvangirai aandamwa na kashfa huku uchaguzi ukikar...: Kituo cha Televisheni cha taifa cha Zimbabwe kimeanzisha kampeni ya kumchafulia jina Morgan Tsvangirai, mpinzani wa rais Robert Mugabe ...

Saturday, July 13, 2013

Tangazo kutoka sekretarieti ya ajira serikalini

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1). Jukumu la msingi la Sekretarieti ya Ajira ni kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma. Hapa ina maana kuwa jukumu la kuajiri, kuthibitisha watumishi kazini pamoja na masuala ya nidhamu ya Watumishi yanabaki kwa Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi katika Utumishi wa Umma mitarafu ya Kifungu cha 6(1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma no 8 ya mwaka 2002. Ambapo katika kuendesha mchakato huo, Sekretarieti ya Ajira inapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, na Taratibu zilizopo ili kuhakikisha Utumishi wa Umma unapata Watumishi weledi na wenye maadili mema. Ambapo hadi sasa jumla ya waombaji 4891 tumeshaendesha mchakato wao wa ajira na kuwapangia vituo vya kazi.
Hata hivyo, Sekretarieti ya Ajira kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipeleka Mswada Bungeni unaopendekeza kukasimu madaraka ya kuendesha mchakato wa Ajira ili baadhi ya Waajiri wakasimiwe madaraka hayo ili kurahisisha utendaji kazi katika kushughulikia mchakato wa ajira kwa baadhi ya kada. Huku Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kuhakikisha kuwa jukumu hilo linaendelea kutekelezwa kwa ufanisi. Tunapoongelea suala la ufanisi hapa Kitengo cha Udhibiti na Ubora kinasimamia suala zima la uhakiki wa taarifa za mhusika, uhakiki wa vyeti na uadilifu wake kwa ujumla. Ambapo hadi sasa tumeshabaini jumla ya vyeti vya kughushi 677 ambavyo wahusika wanadai wamevipata kutoka RITA, VETA na NECTA.
Nafasi wazi za kazi zitakazokuwa zikitangazwa na mchakato wake kuweza kukasimiwa ni pamoja na Kada ya Wasaidizi wa ofisi, Wahudumu wa afya, Madereva, Maafisa Watendaji wa Kata, Mtaa, Kijiji, Wapishi, Walinzi, Madobi, Wasaidizi watunza kumbukumbu pamoja na Makatibu Muhtasi (walio chini ya cheo cha mwandishi mwendesha ofisi) au Kada zingine ambazo Katibu wa Sekretarieti ataona inafaa kukasimu.
1Aidha, nitoe ushauri kwa wanafunzi walioko shuleni na wanaotarajia kuingia vyuoni kuchukua masomo ama kozi za fani ya Afya, Elimu, Mifugo na Kilimo maana ni maeneo ambayo bado yana fursa nyingi za ajira Serikalini na wahitimu wake pindi wamalizapo wanapangiwa vituo vya kazi moja kwa moja bila ya kupitia mchakato wetu wa ajira kutokana na uhaba wa Wataalam wa fani hizo katika soko la ajira hivi sasa.
Sekretarieti ya Ajira katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kwa haraka zaidi zinazohusu mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma, pamoja na kuboresha mawasiliano kati ya Ofisi yetu na wadau ili kuweza kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na duniani kwa ujumla, iliamua kuanzisha tovuti yake (www.ajira.go.tz) ambayo imerahisisha kwa kiasi kikubwa utoaji na upokeaji wa taarifa mbalimbali hususani za matangazo ya fursa za ajira taarifa nyingine zinazohusu masuala ya ajira Serikalini na matangazo mengine yanayohusu shughuli za Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuzinduliwa mwezi Aprili, 2012 imeweza kutembelewa na wadau wapatao 3,017,410
Pamoja na tovuti Sekretarieti ya Ajira imeanzisha KANZIDATA (DATABASE) za aina tatu (3) ambazo ni Kanzidata ya Wahitimu wa Vyuo na Watalaam weledi, Kanzidata ya waliofaulu usaili na Kanzidata ya waliopangiwa vituo vya kazi.
Jambo lingine ambalo ningependa mkalifahamu ni kuwa, Sekretarieti ya Ajira iko katika hatua za awali za mchakato wa kuwawezesha waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi kwa mfumo wa kielektroniki (e-application) kwa nafasi wazi zitakazokuwa zikitangazwa katika Utumishi wa Umma ili kurahisisha kupunguza mlolongo wa uendeshaji mchakato wa ajira ulivyo hivi sasa.
Mwisho nimalizie kwa kuwataka waombaji wa fursa za ajira kutokuchagua maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa vituo vya kazi na Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya kutoa sababu za msingi maana Sekretarieti ya Ajira inaona hili ni kosa na inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu kufanya usaili mwingine waombaji kama hao.



Imetolewa tarehe 12 Julai, 2013 na Riziki V. Abraham, Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma +255-68762497

Thursday, July 11, 2013

Mafuta ya Oki, Viking, Asma sasa marufuku

 
Shirika la Viwango (TBS) limepiga marufuku uuzaji, ununuzi na matumizi ya mafuta ya kula ya aina ya Oki, Viking na Asma baada ya kubainika kuwa hayana ubora na hatari kwa afya za watumiaji.

Kwa mujibu wa Tangazo lilitolewa na Shirika la Viwango nchini (TBS) kwa baadhi ya vyombo vya habari jana, yeyote atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009.

Tangazo hilo lilisema TBS ilinunua mafuta hayo yanayozalishwa nchini Malayasia na kuingizwa kupitia njia za panya, kusambazwa sokoni na kubainika kuwa hayajakidhi matakwa ya kiwango cha kimataifa TZS 559:2010 kinachotumiwa nchini.

“Matokeo ya uchunguzi wa  sampuli  zake  yalibainika kuwa yameshaharibika kabla ya kufikia ukomo wa matumizi kutokana na kutosafishwa ipsavyo, ni  machafu kutokana na kuchanganyika na maji hivyo  vigezo vya ubora wa mafuta havikufikiwa.”

Kwa msingi huo, TBS imewataka wauzaji wa mafuta hayo  kuyaondoa sokoni  mara moja na wateja kuacha kuyanunua hadi hapo itakapothibitika kuwa yamefikia kiwango kinachotakiwa.

Awali  NIPASHE ilichunguza na kubaini kuwa mafuta hayo hushushwa kwenye bandari bubu ya ufukwe wa Mbweni jijini Dar es Salaam na wafanyabiashara ambao pia walidaiwa kukwepa kulipa ushuru.

Kazi hiyo hufanywa bila kificho na baadhi ya waliozungumza na mwandishi wetu walieleza kuwa huenda kuna ushirikiano na maofisa wa vyombo vya dola wasio waaminifu.

Licha ya kukwepa kodi, pia mafuta hayo yamekuwa yakiuzwa kwa bei ya chini kati ya  Sh. 38,000 na  45,000 kwa ujazo wa lita 20 na kuwaumiza wazalishaji wa mafuta ya ndani ambao huuza mafuta ya ujazo huo kwa kati ya Sh.  52,000 na 55,000.

Tofauti hiyo husababisha wenye viwanda  vya ndani kushindwa kufanya biashara kutokana na mafuta hayo kukosa mshindani na kuzagaa sokoni.

Mafuta hayo yamekuwa yakitumiwa kwa wingi na wafanyabiashara hasa wakaanga chipsi kwa vile ndiyo mafuta ya bei nafuu.
CHANZO: NIPASHE